Wakazi wa Kijiji cha Ukimo, Kata ya Mbangamao, Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kuwapatia mradi wa maji safi na salama ambao umemaliza adha ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofadhiliwa na Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wananchi wamesema mradi huo utaboresha maisha yao kwa kiasi kikubwa, huku wakiahidi kuulinda ili uwanufaishe wao na vizazi vijavyo.
Regina Ndunguru, mkazi wa Kijiji cha Ukimo, amepongeza juhudi za RUWASA ngazi ya wilaya na mkoa kwa kutekeleza mradi huo ambao utamaliza changamoto ya kuchota maji kwenye vyanzo visivyo salama na umbali mrefu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ukimo, Kanuni Mbunda, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za mradi huo, akisema upatikanaji wa maji shuleni utaondoa changamoto ya wanafunzi kuafuata maji umbali mrefu.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mbinga, Mhandisi Mashaka Sinkala, amesema mradi huo wenye thamani ya Shilingi milioni 30 umetokana na fedha zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.