• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI Mbinga wapongezwa kwa kuchangia maendeleo

Imewekwa kuanzia tarehe: November 30th, 2021

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Balozi  Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, amefungua zahanati ya kijiji cha Ruanda kata ya Ruanda  katika Halmashauri ya wilaya Mbinga iliyojengwa kutokana na michango ya wananchi,Serikali na wadau wengine wa maendeleo.
Balozi Ibuge, amewapongeza wananchi hao kwa kuamua kutatua kero zao wenyewe bila kusubiri  msaada wa serikali kwa kuchangia Sh. milioni 16 jambo linalopaswa kuigwa na wananchi wa maeneo mengine.
Mkuu wa mkoa alisema, zahanati hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi na kuwataka kuhakikisha wanaitunza na kulinda mindombinu  ili ilete manufaa na kusisitiza kuwa,Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi katika shughuli zote za maendeleo.
Aidha Ibuge, amefurahishwa na kazi nzuri za maendeleo zinazofanywa na wananchi wa wilaya ya Mbinga na kuhaidi kuwa,serikali ya mkoa itaendelea kushirikiana na wananchi walioonyesha jitihada za kumaliza changamoto zao.
Amewataka,viongozi kuanzia ngazi ya vijiji,kata,na Wabunge kujitolea  na kushiriki kazi mbalimbali za maendeleo  zinazolenga kumaliza changamoto na kero  zinazowakabili wananchi.
Diwani wa kata ya Ruanda Deogras Mwingira alisema,wananchi  wa kijiji  hicho waliokuwa wanakabiliwa na kero ya upatikanaji wa huduma za afya kwa kipindi kirefu,sasa wameondokana na changamoto hiyo baada ya kukamilika  kwa ujenzi wa zahanati  hiyo iliyoanza kujengwa tangu mwaka 2013.
Alisema,zahanati hiyo itawapunguzia wananchi wa kijiji cha Ruanda na vijiji vya jirani kero  na adha waliyokuwa wanaipata kwa muda mrefu ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika mengine.

Ameishukuru serikali na wadau waliofanikisha ujenzi huo,kuunga mkono juhudi za wananchi katika kusaidia na kuboresha sekta ya afya kwa wananchi ambao walikaa kwa muda mrefu kusubiri huduma za matibabu.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ruanda Idrisa Machumu alisema,ujenzi wa zahanati hiyo umefanyika kwa awamu tofauti na mpaka kukamilika jumla ya Sh.milioni 91,875,000.00 zimetumika.
Machumu alisema,Halmashauri ya wilaya kupitia mapato yake ya ndani imetoa Sh milioni 25,Serikali kuu imetoa Sh.milioni 50 na wananchi wamechangia Sh.milioni 16,875,000.00 ambapo zaidi ya wakazi 5,700 watanufaika.
Alisema, uwepo wa zahanati hiyo utapunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na kusaidia upatikanaji dawa,vifaa tiba, na vifaa saidizi  kuimarisha na kusogeza huduma za afya kwa wananchi wa kijiji na kata ya Ruanda.
MWISHO.



Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.