Wananchi wa Kijiji cha Mtakanini kilichopo katika Kata ya Msindo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma ya Madaktari bingwa kwa watu wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo, saratani ya kizazi na tezi dume kwenye vituo vya Alafya Wilayani humo.
Shukrani hizo zimetolewa na wananchi wa kijiji cha Mtakanini wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Msindo Mheshimiwa Remna Nchimbi wakati wanampokea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Profesa Mohamedi Janabi ambaye alifika kwenye kituo cha Afya Mtakanini kuungana na Madaktari Bingwa watatu waliokuwa wakiendelea Kutoa huduma kwa wagonjwa kwa magojnwa ya Moyo,Kisukari,Tezi dume na kansa ya shingo ya kizazi kwa akina mama.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mheshimiwa Vita Kawawa amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Mohamed Janabi mara baada ya kuwasili katika kituo cha Afya cha Mtakanini kilichopo kata ya Msindo Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Amesema kitendo cha Serikali kuwaleta madaktari bingwa toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kimeleta matumaini makubwa kwa wananchi ambao wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ambayo yanahitaji kuonana na madaktari bingwa kwa lengo la kupata tiba ambao wako mbali na maeneo ya vijiji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Mohamedi Janabi amesema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata hudua nzuri ya afya kuanzia kwenye zahanati,vituo vya afya ,hospitali za Wilaya na Hospitali za Rufaa ikiwemo hospitali ya Taifa Muhimbili .
Profesa Janabi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo amesisitiza kuwa kila mtu anapaswa kutunza afya yake kwa kula vyakula ambavyo si hatarishi kwa afya jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele ili wananchi waweze kuacha kula vyakula bila kufuata utaratibu.
Ameshauri kuacha kula vyakula vyenye sukari nyingi kwani sukari haija wahi kumuacha mtu salama hivyo ni vyema kuona umuhimu wa kuepuka kula vyakula vyenye sukali nyingi.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa amefurahishwa na kazi nzuri zilizofanywa na Madaktari Bingwa ambao walianza kazi hiyo ya kuwahudumia wangonjwa wa magonjwa ya Moyo,Kisukali,kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake na tezi dume katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Namtumbo na baadae walikwenda Kutoa huduma hiyo kwenye kituo cha Afya Lusewa pia walitoa huduma kwenye vituo vya Afya Mputa na Mtakanini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.