WAKAZI wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,wameiomba Serikali kuhakikisha huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo zzinakua endelea ili kuwafikia wananchi wengi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.
Wametoa ombi hilo ,wakati wa zoezi la uchunguzi na matibabu za magonjwa ya moyo zinazotolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya tiba ya magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) katika Hospitali ya wilaya Namtumbo.
Said Ngonyani,ameomba serikali kupitia Taasisi hiyo kuwa na utaratibu ya kuwawekea kambi ya madaktari bingwa kama hao angalau mara moja kwa mwezi ili wananchi wengi waweze kupata huduma za kitabibu na kupunguza gharama za usafiri kufuata huduma hizo.
Ngonyani amesema,wananchi wengi wanaishi maeneo ya vijijini na vipato vyao ni vidogo na haviwezi kumudu gharama za kufuata huduma za kibingwa katika Hospitali za rufaa,hivyo wengi wao wanajukuta wakiathirika na kupoteza maisha kwa kukosa matibabu ya kibingwa.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya,amewataka wananchi wa Namtumbo kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo kwenda kupata vipimo na matibabu ya magonjwa ya moyo ili kuwa na afya itakayowawezesha kushiriki katika shughuli zao za maendeleo.
Malenya,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Sh.bilioni 1.5 kwa ajili ya uboreshaji wa vituo vya afya katika wilaya ya Namtumbo ikiwemo kituo cha afya Lusewa na Sh.bilioni 1.3 kwa ajili ya kununua vifaa tiba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.