Wananchi wa mjini Mbambabay Wilaya Nyasa mkoani Ruvuma wameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha safari za meli ya abiria ya MV Mbeya II inayoanzia bandari ya Kiwira Kyela mkoani Mbeya hadi Mbambabay Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Wakizungumza kabla ya kupanda meli mjini Mbambabay wananchi wamesema safari za meli ya MV mbeya II ambayo inatoka Kiwira siku ya Alhamis na kuondoka Mbambabay Jumamosi,zinarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wananchi wa mikoa ya Ruvuma Njombe na Mbeya hivyo kukuza uchumi wa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini.
Serikali imenunua meli mpya tatu katika ziwa Nyasa moja ya abiria na mbili za mizigo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.