Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametoa rai kwa wananchi katika tafiti tatu za kitakwimu zinazoendelea hivi sasa ambazo zitawawezesha wao na nchi kupata takwimu rasmi zitakazotumika kutekeleza programu za maendeleo ya kitaifa,kikanda na kimataifa.
Akizungumza na wanahabari kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea,Kanali Thomas amezitaja tafiti tatu ambazo wananchi wanatakiwa kushiriki kuwa ni utafiti wa shughuli za kiuchumi na kijamii wa mwaka 2023/2024.utafiti wa Kilimo wa mwaka 2022/2023 na utafiti wa kutathmini upatikanaji wa huduma za maji,elimu ya afya na usafi wa mazingira wa mwaka 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.