Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka wananchi kuachana na matumizi ya kuni na badala yake kutumia nishati mbadala kwa ajili ya kupikia ili kudhibiti uharibifu wa mazingira, kupunguza hatari ya jangwa, na kuhifadhi uoto wa asili.
Kapenjama amesema haiyo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Songea (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa HOMSO Songea.
Wadau mbalimbali walihudhuria kikao hicho kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa kazi kupitia halmashauri za Madaba, Songea, na Manispaa ya Songea.
Miongoni mwa sekta zilizojadiliwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya nishati mbadala kama makaa ya mawe, mikakati ya kudhibiti utoro wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari, na udhibiti wa ufugaji holela wa ng’ombe.
Afisa Misitu wa Manispaa ya Songea, Betram Njelekera, amesema kuwa kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita, Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini amewezesha vikundi 12 kwa kuwagawia mama lishe mitungi 84 ya gesi ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.