Wananchi wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwajengea kituo cha Afya Masonya.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Masonya kilichojengwa katika Tarafa ya Mlingoti.
Ziada khalifa ni Afisa mtendaji amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajengea kituo hicho kwani kitawapunguzia changamoto ya umbali wa kufuata huduma njee ya tarafa na asa kipindi cha mvua kimekuwa kelo kwa wajawazito
“Saizi tunajua tumeshapata kituo cha Afya tunaamini changamoto zitapungua kwasasabu hudama itakuwa ipo karibu kwa kweli atuamini na sisi leo kama tumejengewa kituo Kijijini kwetu tunaishukuru Serikali kwa kutuona”alisema khalifa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, amewataka wananchi hao kuusimamia mradi huo na amemtaka mkurugenzi kuhakikisha anapeleka maji na umeme kwa wakati na kuboresha miundo mbinu yote katika kituo hicho
“Huu ni mradi ambao ujenzi wake unatekelezwa na fedha za tozo lakini kumekuwa na watu ambao wanashirikiana na Wajenzi kuiba vifaa viliyo nunuliwa kwajili ya mradi kwahiyo tukiruhusu hiyo hali tunajikomoa sisi wenyewe kwa kukwamisha maendeleo yetu naomba tuisimamie kwa dhati” alisema Thomas.
Ujenzi huo unaendelea ambapo jengo la OPD na Maabara yamekamilika na mengine yakiwa hatua ya mwisho pia ujenzi umegharimu shilingi Milioni 500 ambapo Fedha hizo zitokana Tozo za miamala ya simu ambapo halmashaurizote za mkoa wa Ruvuma vimepata gawio hilo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.