Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo amekabidhi pikipiki katika kituo cha polisi Litembo iliyogharimu shilingi milioni 2,000,000.
Hafla ya kukabidhi pikipiki hiyo imefanyika katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga.
Afisa Tarafa wa Mbuji Salma Kipande akizungumza kwenye hafla hiyo amesema wananchi wamechangia shilingi milioni mbili ili kununua pikipiki hiyo.
Amelitaja lengo la kununua pikipiki hiyo ni kutambua changamoto wanazopitia askari wa kituo cha polisi Litembo ili kuwafikia na kuwapatia huduma kwa wakati kukabiliana na uharifu.
Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga amewapongeza wananchi kwa kuona kituo cha polisi Litembo kinatoa huduma kwa wakati .
“pikipiki hii itasaidia kukabiliana na vitendo vya uharifu na kuyafikia maeneo ya tarafa ya Mbuji kwa wakati .
Hata hivyo ametoa rai kwa kituo hicho kuitumia pikipiki hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbinga SP Elias Fungo, amewashukuru wananchi hao kuwasaidia kupata pikipiki hiyo, ambayo itawasaidia katika utendaji kazi wa kufuatilia taarifa za uharifu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.