Wananchi wa Kata ya Mpepo Wilayani nyasa mkoani Ruvuma wameipongeza Serikali Kwa kutatua changamoto ya barabara ya Luhindo- Mpepo hadi Darpori ambayo imetengezwa Kwa kiwango Cha changarawe hivyo kupitika muda wote.
Wananchi hao wameyasema katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mpepo na kuongozwa na MKuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Filberto Sanga.
Wananchi wamesema barabara ya awali ilikuwa haipitiki na walikuwa wakitumia gharama kubwa za usafiri ambapo hivi sasa mabasi ya abiria yanafika kijijini hapa kwa gharama nafuu.
Wamempongeza Rais Dkt Suluhu Hassan Kwa kutatua kero ya barabara na umeme kero ambazo zimewawasumbua wananchi kwa muda mrefu.
Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa TARURA wilaya ya Nyasa Mhandisi Thomas Kitusi amesema Ujenzi wa barabara ya Luhindo-Mpepo- Darpori Kwa kiwango Cha changarawe imetekeleza Kwa kutumia fedha ya Mfuko Maalum kiasi cha shilingi milioni 750 zilitengwa.
Amelitaja lengo la mradi huo ni kuboresha mawasiliano na huduma Kwa wananchi na kuunganisha wilaya ya Nyasa na nchi jirani Msumbiji.
Akizungumza kwenye mkutano huyo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Filberto Sanga amewapongeza TARURA kwa kutekeleza mradi huo hivyo kumaliza kero ya ubovu wa barabara.
Amewaasa wananchi kuitumia barabara hiyo kujiletea maendeleo yao ili kukuza uchumi wao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.