Wananchi wa Kijiji cha Mtyangimbole, kata ya Mtyangimbole, Halmashauri ya Madaba, wilayani Songea mkoani Ruvuma wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan , kwa ujenzi wa shule ya sekondari katika eneo hilo.
Shule hiyo imeondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali wa zaidi ya kilomita nne kufuata elimu, hatua inayowaongezea muda wa kupumzika na kujisomea.
Mkazi wa kijiji hicho, Jackson Lomanus Luambano, amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo umeleta faraja kubwa kwa jamii kwani wanafunzi sasa wanapata elimu katika mazingira bora.
Wananchi wamempongeza Rais Samia kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu, ambayo imekuwa chachu ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Madaba, Mhe. Joseph Kizito Mhagama, katika ziara yake ya kikazi, amewataka wananchi kutokubali kulaghaiwa na watu wanaobeza juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu.
Amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika ujenzi wa shule, akisisitiza kuwa haya ni matokeo ya juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake.
Ameeleza kuwa Halmashauri ya Madaba inajivunia kuwa kinara kitaaluma katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.