Waumini wa kanisa la Wasabato Madaba na wanafunzi wa chuo cha Afya Songea (Songea College ofa health and allied science) wamechangia damu katika hospitali ya Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma
Katika zoezi hilo jumla ya chupa 19 za damu zimetolewa kwaajili ya uokoaji wa wagonjwa wa dharura, na huduma za mama na mtoto.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mussa Rashid amewapongeza waumini wa kanisa hilo na wanafunzi wa chuo cha Afya Songea kwa kujitoa kutoa damu na kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi wengine.
“Uchangiaji wa damu salama ni hiari na ni muhimu kwa sababu katika hospitali yetu tunauhitaji mkubwa wa damu ili kuokoa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji ikiwa huduma za mama na mtoto zinaendelea,uhitaji wa damu salama ni mkubwa”.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.