NAIBU Waziri Wizara ya maliasili na utalii Mheshimiwa Mary Masanja, amefanya ziara mkoani Ruvuma katika wilaya ya Namtumbo, lengo likiwa kutembelea chuo cha mafunzo maliasili na jamii.
Akizungumza wakati akizindua ukumbi wa mkutano na maktaba katika chuo cha mafunzo maliasili na jamii kilichopo Likuyu Sekamaganga, Alisema elimu inayotolewa chuoni hapo ikawe msaada kwa wananchi wanao ishi pembezoni mwa hifadhi.
”Nimefurahi kusikia kuwa chuo hiki kinatoa mafunzo wa uhifadhi wa maliasili na jamii, pia niwaombe kama chuo msihishie kutoa elimu kwa wanafunzi bali hadi kwa wananchi wanao ishi karibu na hifadhi kwa maana wajue namna ya kujilinda wanyama pori kwani itasaidia kupunguza maafa kwao” alisema Mary.
Hata hivyo amesisitiza kuwa lengo serikali kuanzisha chuo hicho ni kuielemisha jamii namna ya kutunza mazingira lakini pia itaongeza ajila kwa vijana, pia italaisisha jamii ipende utalii na kujua namna ya kuwakwepa wanyama pori
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.