• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI waridhia kuvunja nyumba kupisha ujenzi wa barabara Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: August 17th, 2022

WANANCHI wanaoishi kando kando ya barabara ya Kitai-Luanda- Lituhi inayojengwa kwa kiwango cha lami na wakala wa barabara Tanroads mkoa wa Ruvuma,  wameanza kuvunja nyumba zao kwa hiari ili kupisha  kazi ya ujenzi wa barabara hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema,wameamua kuvunja nyumba zao kwa kuwa mradi huo ni muhimu kuliko hata nyumba zao kwani kwa muda mrefu walikuwa wanapata mateso makubwa  ya usafiri  ,usafirishaji wa bidhaa na madhara ya kiafya.

Halfan Nambasi  mkazi wa kijiji cha Amani makolo alisema,kile kinachofanywa na serikali kina thamani kubwa kuliko nyumbani zao, na ameipongeza sana serikali kupitia Tanroads mkoa wa Ruvuma kwa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwani.

Alisema,kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutaharakisha sana kukua kwa uchumi na kupungua kwa gharama ya usafiri kwa wananchi na usafirishji wa mizigo.

Nambasi alisema,barabara hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa vijiji mbalimbali kwa sababu licha ya itakwenda kuharakisha kukua kwa uchumi wa vijiji hivyo, itahamasisha  wawekezaji wengi kwenda kuwekeza katika madini yanayopatikana kwa wingi katika ukanda huo.

Aidha,ameiomba serikali kupitia Tanroads kuwa karibu na mkandarasi ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na ajenge kwa viwango ili kuepusha usumbufu unaoweza kutokea wa kufanya matengenezo ya mara kwa  mara.

Alisema,barabara hiyo ndiyo uti wa mgongo kwa uchumi wa wilaya ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma kwa sababu barabara ndiyo inayotumika kupita malori shehena ya makaa wa mawe kutoka kwenye migodi  kwenda  maeneo mbalimbali hapa nchini.

Osias Haule alisema, kwa muda mrefu walikuwa  katika mateso na  kupata madhara makubwa kiafya kutokana na vumbi kubwa linalotoka barabarani na kuingia majumbani pindi malori ya makaa ya mawe yanapopita na kuna baadhi ya watu wamepoteza maisha yao kwa sababu ya kutojua njia sahihi ya kujkinga na vumbi la makaa ya mawe.

Alisema,baadhi ya wananchi walichukia uwekezaji huo licha ya kuwa na manufaa makubwa yanayopatikana,lakini hawana uwezo wa kuzuia magari yasipite katika bara bara hiyo bali waliendelea kuumia huku wakimuomba Mungu awanusuru na mateso hayo.

Alisema, mara baada ya kuona serikali imeanza kujenga kwa lami  sasa wananchi wengi wana furaha na  kwa kuwa  baada ya muda mfupi wataondokana na  kero hiyo na kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa  hatua hiyo.



Benedict Haule mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Amani makolo alisema, hiyo ni hatua kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo na wilaya ya Mbinga kwa ujumla na amewaomba wananchi ambao bado hawajabomoa nyumba zao kufanya hivyo ili  kupisha kazi  ya ujenzi ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa.



Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo kutoka wakala wa barabara mkoa wa Tanroads mkoa wa Ruvuma Andrew Sanga alisema,barabara hiyo inajengwa na kampuni ya China Ralway Seventh Group Ltd(CRSG) kutoa nchini China.



Alisema,katika awamu ya kwanza itajengwa urefu wa km 35 kwa kiwango cha lami kutoka kijiji cha Amani makolo hadi Luanda,lakini katika mpango wa baadaye serikali inakusudia kujenga barabara hiyo  hadi Lituhi.


Alisema,kwa sasa kazi inafanyika katika kipande cha Kitai kuelekea Luanda ambapo katika hatua ya awali mkandarasi ameanza  kusafisha barabara na kuondoa udongo usiohitajika.



Alisema, mradi huo utahusisha  ujenzi wa madaraja makubwa matano na madaraja mengine madogo kama sabini, ambapo kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kunakwenda kufungua shughuli za kiuchumi kwa wananchi na kumaliza kabisa changamoto ya usafiri iliyopo hivi sasa.


Alisema,kazi inakwenda vizuri na kasi ya mkandasari ni kubwa na mara barabara hiyo itakapokamilika itasaidia sana kiuchumi ikiwamo usafirishaji wa makaa ya mawe na kuongezeka kwa wawekezaji kwenye sekta ya madini ya makaa ya mawe.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.