wananchi zaidi ya 2,206,169 kutoka mikoa ya Ruvuma, Njombe, Mtwara, na Lindi wamepata elimu ya sheria kupitia mabanda yaliyokuwa katika Soko Kuu Songea na vipindi vya redio za kijamii.
Hayo yamesemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa James Karayemaha wakati anazungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini iliyoanza 25 Januari 25,2025 na kufikia tamati Februari Mosi 2025.
Mheshimiwa Karayemaha amesema Wiki ya sheria imelenga kupunguza hofu dhidi ya mfumo wa mahakama, majaji, mahakimu, polisi, na taasisi za kupambana na rushwa.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu:
“TANZANIA YA 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.”
Jaji Mfawidhi amesisitiza umuhimu wa misingi ya haki na amani katika maendeleo ya taifa. Pia, amezitaka taasisi za haki madai kushirikiana kwa karibu kuhakikisha mfumo wa sheria unachangia kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
Wadau waliotoa mchango mkubwa katika wiki ya sheria ni pamoja na Jeshi la Magereza, Polisi, Mawakili wa Serikali, TLS, TAKUKURU, Zimamoto, Uhamiaji, Vodacom, NMB, NBC, na taasisi nyingine nyingi.
Wadau hawa walihamasisha matumizi ya TEHAMA katika mfumo wa sheria, ikiwemo usajili wa mashauri kwa njia ya mtandao (e-CMS), usikilizaji wa mashauri kwa video conferencing, na mfumo wa TanzLII kwa upatikanaji wa nyaraka za kisheria.
Mahakama ya Tanzania imeahidi kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili kufanikisha utoaji wa haki kwa haraka na kwa uwazi. Aidha, imesisitiza matumizi ya usuluhishi (mediation) kama njia mbadala ya kutatua migogoro kwa haraka, kuokoa muda na gharama za mashauri.
Miongoni mwa changamoto zilizotajwa zinazoweza kuathiri utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050 ni pamoja na Ucheleweshaji wa mashauri,Rushwa na vitendo vya ukiukwaji wa maadili,Ukosefu wa elimu ya sheria kwa wananchi,Kukosa weledi katika kushughulikia migogoro ya walipa kodi na Ukosefu wa majengo ya mahakama na watumishi wa kutosha.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mheshimiwa James Karayemaha, amehimiza jamii kushiriki katika uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, akisisitiza kuwa maendeleo na ustawi wa jamii hayawezi kupatikana bila haki na amani.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.