MKUU wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amewataka wananchi wilayani humo kuwafichua wahujumu wanaorudisha nyuma juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kumtua mama ndoo kichwani wanaoiba miundombinu ya maji.
Mgema alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati alipokuwa akifungua kongamano la michezo lijulikanalo Maji Cup lenye lengo la kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo na kulinda upotevu wa maji lililofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini humo.
Mgema alisema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiiba na kuharibu miundombinu hiyo hususan mabomba ambayo imetengenezwa kwa kutumia fedha nyingi za serikali na wahisani na kusababisha akina mama wengi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Aidha amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kuendesha shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji kwa madai kwamba wanasababisha ukame na kupelekea vyanzo vya uzalishaji wa nishati ya umeme kukosa huduma hiyo.
Alifafanua kuwa huduma ya maji ni muhimu kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuendesha mitambo ya ufuaji wa nishati ya umeme pamoja na kusaidia maisha ya Bianadamu,viumbe hai na kilimo.
Naye Diwani wa kata ya Mjini iliyopo katika Halmashauri ya manispaa ya songea mkoani humo Mathew Ngalimanayo akizungumza kwenye kongamano hilo amewataka wananchi hao kuenzi mchango wa wazee wetu wa zamani katika suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na kuwahasa waachane na mambo ya utanda wazi ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu huo wa mazingira na kupelekea uwepo wa mabadiliko ya hali ya hewa(TABIANCHI)
Kwa upande wake Afisa mahusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya Songea(SOUWASA)Paulo Mandia alisema kuwa kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na ATAWASI na kushirikisha timu ya Mandera Veterani,Mji Concine,SOUWASA na Mwanawasa kwa lengo la kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo na kuzuia upotevu wa maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.