Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WEF) umetoa mkopo zaidi ya shilingi milioni 287 tangu mwaka 2015 hadi 2024 Kwa wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na , Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya wakati anazungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya mwanamke Duniani kiwilaya kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Nasuli.
Malenya amelitaja kundi la wanawake kuwa ni nguvu kazi kubwa kulingana na wingi wao.
Hata hivyo amesema wanawake wamekuwa wakinyanyashwa, kukandamizwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili.
"Nawaasa wanangu wa jinsia ya kike endeleeni kuchukuwa tahadhari hakikisheni wale wanaume wanaowamendea wasiwapate, tunataka nyinyi muwe sehemu ya ushuhuda wa awamu ya Sita kwa maendeleo ya mwanamke ". amesema Malenya.
Ametahadharisha kuwa wilaya ya Namtumbo imeathiriwa Kwa janga la UKIMWI ambapo takwimu zinaonesha kuwa wanawake walioathirika idadi yao ni kubwa kuliko wanaume.
Ametoa rai kwa Taasisi za kifedha kuendelea kuboresha huduma rafiki katika kuwafikia wanawake wengi na kuwapa mikopo yenye riba nafuu
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Namtumbo Peresi Kamugisha amesema Serikali imewekeza katika afya Ili kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua na kwamba serikali imeimarisha miundo mbinu ya shule maalumu za watoto wa kike katika wilaya ya Namtumbo.
Kwa upande wake Afisa USTAWI wa Jamii wilaya ya Namtumbo Frida kayombo amesema ukatili wa kijinsi ni matumizi mabaya ya nguvu na huleta madhara kimwili, kiakili.
Naye Mhamasishaji wa Damu Salama Wilaya ya Namtumbo Godfrey Mwaulesi amewaomba wakinamama kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo la damu kama wakinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi na watu wanaopata ajali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.