Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wanatarajiwa kuhudhuria kongamano maalum litakalofanyika Machi 3,2025 katika Ukumbi wa Bombambili Manispaa ya Songea kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Kongamano hili limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayowahusu wanawake, ikiwemo ukatili wa kijinsia, msaada wa kisheria, ujasiriamali, na malezi.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.
Wanawake wote wa Mkoa wa Ruvuma wamealikwa kushiriki katika kongamano hilo, ambalo litatolewa bila malipo yoyote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.