KUFUATIA Wiki ya Wanawake Duniani wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wametembelea Kitua cha Upendo cha kulelea watoto wanaishi katika mazingira magumu.
Akizungumza Mwenyekiti wa wanawake katika Ofisi hiyo Amina Tindwa amesema katika kuadhimisha wiki ya Wanawake Duniani wanatembelea vituo mbalimbali za wahitaji ikiwa mwanamke ni mlezi katika familia.
Hata hivyo amesema mahitaji waliyopeleka katika kituo hicho ni mbolea pamoja na bidhaa zingine zimegharimu kiasi cha shilingi Laki nne na ishiri na tano(425,000/=).
Sista Benigina Kapinga kutoka shirika la Utatu Mtakatifu amesema kituo hicho kina watoto 24 ambao mmoja yupo chuo na wengine Sekondari pamoja na wengine shule ya msingi na awali.
Kapinga amewashukuru wanawake hao kwa moyo wa upendo ikiwa misaada hiyo hupata mara chache na kinachopelekea kukosa misaada hiyo kuto sajiliwa kwa kituo hicho.
Afisa Maendeleo Jamii Mkoa wa Ruvuma Exerveria Mlimila ameshauri Mkuu wa kituo hicho kufanya jitihada ya kusajili ili kitambulike na kufikia kupata misaada mara kwa mara na kuweza kukidhi mahitaji ya watoto hao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Marchi 3,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.