Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Musa Mumina, amewataka waratibu na wasimamizi wa lishe kuongeza juhudi katika kutoa elimu ya lishe kwa wananchi ili kuboresha afya na ustawi wa jamii.
Akizungumza katika kikao kazi na wadau wa lishe, Ndg. Mumina alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu lishe bora na matumizi sahihi ya vyakula vinavyopatikana kwa wingi katika mazingira yao. Alieleza kuwa lishe duni imechangia matatizo ya afya kama utapiamlo, udumavu kwa watoto, na magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha, aliwataka maafisa lishe kushirikiana na viongozi wa jamii, watoa huduma za afya, na taasisi za elimu ili kufanikisha mpango wa utoaji wa elimu ya lishe kwa wananchi wote, hususan kwa makundi maalum kama watoto, wanawake wajawazito, na wazee.
Ndg. Mumina alisisitiza kuwa juhudi hizi zinapaswa kuungwa mkono kwa vitendo kwa kuhakikisha wananchi wanapata mafunzo kuhusu vyakula vyenye virutubisho vya kutosha kama mboga za majani, matunda, nafaka, maharagwe, samaki, nyama, na vyakula vya asili ambavyo vinaweza kuboresha afya zao kwa gharama nafuu.
Mwisho, aliwataka waratibu wa lishe kuhakikisha wanazingatia mipango madhubuti ya kitaifa kuhusu lishe na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa elimu ya lishe inawafikia wananchi wengi kwa njia rahisi na endelevu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.