WARATIBU wa Kanda 8 za mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wamepatiwa mafunzo ya siku moja katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Mratibu wa mafunzo ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo John Mwakisulu aliwaambia waratibu wa Kanda kutumia mafunzo hayo kwenda kuelimisha jamii kupitia mikutano ya hadhara Ili zoezi la unjweshaji dawa lisiwe gumu Kwa jamii.
Mwakisulu amesema uelimishaji wananchi kuhusu magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni Jambo muhimu Ili waweze kujua umuhimu wa kupata Tiba .
Mwakisulu aliwataja waratibu wa Kanda kuwa ni Nurdin Galasi Kanda ya Mputa, Peter Ndunguru Kanda ya Lusewa, George Kinyaga Kanda ya Msindo, Ditto Zabron Kanda ya Litola, Victoria Lugongo Kanda ya mkongo,Josephina Magingo Kanda ya Likuyuseka ,Joseph Hokororo Kanda ya Namtumbo pamoja na Abel Godson Kanda ya Ligera.
Shaibu Majiwa mratibu wa afya idara ya elimu aliwataka waratibu wa Kanda kutopika taarifa na badala yake watoe taarifa sahihi Ili kujua halihalisi ya wilaya ya Namtumbo katika magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
"Upikaji wa taarifa katika zoezi hili halitatupa halihalisi ya tathmini ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika wilaya ya Namtumbo alisema Majiwa.
Rajabu Chiukuta Kaimu mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Ruvuma aliwataka waratibu wa kanda kutumia mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha wananchi Ili wauelewe mpango na kurahisisha zoezi la kuwapatia dawa.
Peter Ndunguru mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Kanda ya Lusewa alisema nguvu nyingi katika kutekeleza mpango huu zielekezwe kwenye kuelimisha jamii ielewe na kudai kuwa jamii ikishs elewa zoezi la mpango huu litakuwa rahisi.
Waratibu wa Kanda 8 pamoja na kupatiwa mafunzo hayo wamepatiwa vifaa Tiba na dawa Kwa ajili ya kwenda kutekeleza mpango katika jamii wilayani Namtumbo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.