Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI imeendesha mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa wasimamizi ngazi ya Mkoa wa Ruvuma na Halmashauri zote nane wanaohusika na mfumo wa uagizaji dawa,vifaatiba na vitendanishi.
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea yamefunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jeremiah Sendoro.
Mafunzo yamelenga kuwaelimisha wasimamizi ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhusu mwongozo wa mfumo wa mshitili ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2018 na Wizara ya Afya lengo likiwa ni kuhakikisha wadau wote wanafuata mwongozo wa mshitili kwenye uagizaji dawa,vitendanishi na vifaa tiba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.