Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo amewataka wataalam wa afya wa Hospitali ya Mkoa kufanya kazi kwa weledi, uzalendo na kujituma ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wataalam hao katika ukumbi wa mikutano uliopo katika hospitali hiyo mjini Songea.
Ameongeza kuwa wao kama watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa umoja ili waweze kutoa tiba sahihi kwa ajili ya wananchi.
"Nitambue na kuwapongeza sana kwa majukumu makubwa na ya kipekee ya kuwahudumia watanzania na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma".
Makondo ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuendesha huduma, miundombinu, vifaa tiba, ujenzi pamoja na maboresho ili kuhakikisha huduma zinatolewa katika mazingira bora.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dr.Magafu Majura kwa niaba ya watumishi wa hospitali hiyo amemshukuru Katibu Tawala kwa Ziara hiyo na ameahidi maelekezo yote aliyoyatoa kuyafanyia kazi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.