Wataalam wa mifugo Nyanda za Juu Kusini wameweka mikakati endelevu itakayosaidia kudhibiti magonjwa ya mifugo na kukuza uchumi na pato la Taifa.
Mikakati hiyo imewekwa na wataalam hao katika Kikao cha wataalamu wa uvuvi na Mifugo kanda ya Nyanda za Juu kusini kilichojumuisha mikoa mitano ya Iringa,Mbeya,Njombe,Ruvuma na Songwe na kufanyika kwenye ukumbi wa Songea klabu mjini Songea.
Akizungumza wakati anafungua kikao hicho mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Uchumi na Uzalishaji n Jeremia ameyataja malengo ya kikao hicho kuwa ni kujadili mikakati na changamoto katika sekta ya ufugaji na Uvuvi.
Amesema changamoto zikipatiwa ufumbuzi wa kudumu zinaiwezesha sekta ya mifugo na uvuvi kusonga mbele na iweze kufanya vizuri kwa kuinua pato la mtu mmoja mmoja na kuinua Uchumi wa Nchi.Sendoro amewapongeza Maafisa Mifugo na Uvuvi kwa kazi kubwa wanazofanya ,licha ya Halmashauri zote kuwa na uhaba wa maafisa ha ukilinganisha na mahitaji ya yaliyopo ambapo ametoa rai waendelea kupambana na kuhakikisha sekta ya mifugo inasonga inapata mafanikio makubwa.
Hata hivyo Katibu Tawala Msaidizi huyo amesema katika Sekta hiyo kuna tatizo la magonjwa ya mifugo na kwamba mwananchi wa kawaida anategemea wataalamu wa mifugo kuwapa elimu sahihi na kuhakikisha Mifugo inakuwa na afya nzuri.
“Kuna magonjwa yanayomaliza baadhi ya mifugo mfano kideri NA mdondo yanasababisha kuku kufa, kwa mwaka huu katika Mkoa wa Ruvuma kuku zaidi ya laki moja wamekufa”,alisema Sendoro.Amewaomba wataalamu wa Mifugo kuhakikisha mifugo inaposafirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine wahakikishe wanachukua sampuli ili kujiridhisha vinginevyo ugonjwa utasambaa sehemu moja kwenda nyingine.
Sendoro amewashauri wataalamu wa mifugo kuchukua tahadhali ili kuhakikisha afya ya mifugo inakuwa salama na mfugaji hapati hasara na kupata mbegu bora za mifugo.Kwa upande wake Daktari wa mifugo wa Mkoa wa Mbeya Samora Stanley akizungumza katika kikao hicho ametoa rai kwa wafugaji kuangalia namna ya kutatua changamoto mbalimbali inayoikabili sekta hiyo.
Meneja wa wakala wa Maabara Nyanda za Juu Kusini Dr.Kwali Bula amesema wameanagalia namna bora ya kudhibiti Magonjwa ya mifugo pamoja na kutoa chanjo na uogeshaji wa mifugo.Amesema kila Halmashauri wamejiwekea utaratibu wa kuchanja mifugo na ukusanyaji wa Maduhuri wa Serikali za Mitaa pamoja na Serikali kuu kutoka kwa wataalamu wa kanda kutoka iringa, ambayo inategemewa zaidi kwa wanyama kama Nguruwe na Ngómbe wa Maziwa.
Imeandaliwa Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 28,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.