WATALII 15 kutoka nchini Ujerumani wakiongozwa na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini nTanzania Mheshimiwa Till Vnorn wametembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea ambapo waliweza kupata historia ya mashujaa 67 wa vita ya Majimaji waliouawa kikatili na wajerumani mwaka 1906.
Watalii hao waliotembelea makaburi mawili moja walizikwa mashujaa 66 na kaburi la pili ambalo alizikwa Jemedari wa Kabila la wangoni Nduna Songea Mbano amb aye alizikwa kwiliwili bila kichwa kwa kuwa wajerumani baada ya kuumua Nduna Songea walikata kichwa chake na kukipeleka nchini Ujerumani ambacho kimehifadhiwa hadi leo.
Ziara ya wageni hao kutoka Ujerumani imelenga zaidi kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Ujeruamni na kujifunza historia kati ya Tanzania na Ujerumani ambayo imelenga kufungua fursa mpya za utalii na uwekezaji kwa vijana wa Tanzania na Ujerumani
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.