Wateja watano wa Benki ya NMB wamejinyakulia fedha taslimu Sh.milioni moja kila mmoja katika Droo ya kila Mwezi iliyochezwa katika tawi la NMB Songea kupitia kampeni kubwa inayofahamika kwa jina la Pesa Akaunti.
Wateja walioshinda Droo hiyo ya mwezi ni Alhami Shemkay ,Msimu Mwnyimvua, Abdala Msimu, Emanue Masawe ,na unior Mtweve.
Pesa akaunti ni Droo maalum inayoendeshwa na Benki hiyo ikihamasisha Watanzania kutumia Benki ya NMB kuweka fedha,kufungua akaunti,na kupata mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo.
Meneja wa mauzo wa NMB Kanda ya kusini Roman Degeleki amesema,akaunti ya Pesa Akaunti inafunguliwa kwa gharama ndogo kuanzia Sh.1,000 na haina kianzio cha fedha na mteja hapewi kadi badala yake anaunganishwa moja kwa moja na simu yake ya mkononi.
Amesema,akaunti hiyo inamwezesha mteja kufanya matumizi na malipo mbalimbali ikiwemo kulipa Luku,kununua King’amuzi,kulipa bili za maji na vitu vingine kulingana na mahitaji ya mteja husika
Kulingana na Meneja huyo,kupitia Pesa akaunti mteja anaweza kuchukua mkopo hadi Shilingi laki tano kupitia simu yake ya mkononi bila kuweka dhamana yoyote na kurejesha mkopo huo kwa kutumia simu yake.
Degeleki ametaja,faida nyingine ya Pesa akaunti kuwa ni mteja kupata Bima ya simu ambayo ikipata changamoto yoyote Benki ina uwezo wa kuifanyia matengenezo simu hiyo bila kujali gharama zake.
Ametoa rai kwa Watanzania,kuchangamkia fursa hiyo kwa kuendelea kufungua akaunti na kuweka fedha kwenye Benki ya NMB ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa katika kila Wilaya na Mkoa hapa nchini.
Kaimu meneja wa NMB Tawi la Songea Mwalimu Mbwambo amesema,Droo ya mwezi imewahusisha wateja ambao waliweka fedha kwenye akaunti zao kuanzia kiwango cha fedha kisichopungua Sh.50,000.
Kwa upande wake Mkaguzi na Mdhibiti wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Salim Bugufi amesema,kampeni hiyo inafanyika chini ya uangalizi wa Bodi hiyo ili kujiridhisha mtu anayepata fedha hizo kuwa ni mteja halali ya NMB.
Mkazi wa kijiji cha Ligera wilayani Namtumbo Silaji Mango,ameipongeza Benki hiyo kwa kuendesha Droo hiyo ambayo imehamasisha watu wengi kutumia Benki ya NMB kwa kufungua akaunti na kuweka fedha.Mango,amewasihi washindi wa Droo hiyo kutumia fedha walizopata kuwekeza katika shughuli muhimu za maendeleo kama vile kilimo na mifugo badala ya kuzitumia kwenye mambo ya anasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.