Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo amewaagiza watendaji Kata katika Halmashauri kutekeleza afua za lishe kwa kuielimisha na kuihamasisha jamii kutambua umuhimu wa lishe ili kukabiliana na udumavu.
Mangosongo ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe kwa kipindi cha robo ya pili ya utekelezaji wa afua za lishe kilichowashirikisha wadau wa lishe na watendaji kata na kufanyika mjini Mbinga.
Amewataka watendaji kata kuhakikisha wanatoa elimu na hamasa hasa kwa wanaume ili waweze kutambua lishe na kushiriki maadhimisho ya siku za lishe za vijiji na kata.
“Elimu ya lishe sio kwa wanawake na watoto tu,ni wakati wetu sasa kuhakikisha wanaume pia wanashiriki na kupata elimu ya lishe ili kuimarisha afya za Jamii yote ”,alisisitiza.
Ameagiza kuhuishwa kwa sheria ndogo za vijiji zinazowabana wazazi wenye watoto kushiriki utekelezaji wa afua za lishe pamoja na kuwapeleka kliniki kwa ajili chanjo. Amesisitiza ufuatiliaji wa karibu,kutoa elimu na kuchukua hatua dhidi ya watoto wanaozaliwa na uzito pungufu pamoja na utapiamlo mkali.
Ametoa rai kwa wadau wa lishe kuhamasisha wadau wenye mashine za kusaga nafaka kufunga kifaa cha kuongeza virutubisho kwenye unga na kuhakikisha kila shule inaanzisha klabu za lishe na bustani za matunda na mboga.Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na udumavu nchini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.