Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma imeanza rasmi mafunzo maalum ya moduli ya Kodi ya Majengo na Kodi ya Mabango kwa watendaji wa kata na vijiji, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo hivyo muhimu.
Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo na yamezinduliwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Sajidu Idrisa Mohamed.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkurugenzi huyo amewahimiza washiriki wote kuzingatia kwa makini kila somo linalotolewa kwa kuwa lina mchango mkubwa katika kuhakikisha Halmashauri inakusanya mapato kwa ufanisi.
Alisisitiza kuwa mafanikio ya zoezi hilo yanategemea uzingatiaji na uwajibikaji wa watendaji katika kutekeleza majukumu yao.
“Nasisitiza kila mtendaji atambue idadi ya vitongoji, majengo na wamiliki wa majengo katika kijiji chake. Hakikisheni hakuna jengo linalobaki bila kusajiliwa,” alisema
Zoezi la ukusanyaji wa taarifa za majengo na mabango linatarajiwa kufanyika kwa siku 14 mfululizo.
Watendaji waliopata mafunzo hayo watatumia teknolojia ya kisasa ikiwa ni pamoja na mfumo wa TAUSI na programu tumishi ya ODK kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kutoka maeneo ya vijijini.
Kupitia mafunzo hayo, Halmashauri ya Madaba inalenga kuongeza uwezo wa watendaji wake katika kusimamia vyanzo vya mapato,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.