Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Wakili Mtatiro amewaagiza watumishi wa serikali kwenye vijiji na Kata kuwafikia wananchi ili kusikiliza kero na kuweza kuzitatua kwa kuzipatia suluhisho la kudumu.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Matemanga kwenye mkutano wa hadhara Mheshimiwa Mtatirro amesema wananchi wanakabiliwa na kero mbalimbali kwenye maeneo hayo hivyo ni vema watumishi wa umma kuwajibika na kwenda kuwasikiliza badala ya kumsubiri Mkuu wa Wilaya.
Mtatiro amewasisitiza wananchi kuongeza mashamba ili kuweza kuongeza tija kwenye mazao na kuongeza uchumi wa mtu mmoja na serikali kupata mapato. .
“Tuwekeze nguvu kuandaa mashamba ili kuongeza uzalishaji wa mazao, itasaidia kuongeza faida, kila unapohudumia shamba lako kikamilifu tarajia kupata mazao ya kutosha'',alisistiza DC Mtatiro.
Mkuu wa Wilaya pia amewataka wazazi ambao bado hawajawapeleka watoto wao shule wawapeleke mara moja ili waweze kupata haki yao ya elimu ambapo amesisitiza operesheni ya kuwakamata wazazi ambao bado hawajawapeleka shule watoto wao itafanyika nyumba hadi nyumba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.