Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma Mheshimiwa Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Aajira na Wwenye ulemavu amewataka wazazi kulinda watoto dhidi ya utandawazi ambao unaharibu mila, desturi na maadili.
Ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Litowa Kata ya Parangu.
“Unyanyasaji wa watoto umeongezeka sana zamani tulikua tunaangaika kulinda watoto wa kike lakini sasa hivi hadi watoto wadogo wa kiume wananyanyasika na kufanyiwa vitendo vya kikatili hivyo nawasihi wazazi wenzangu tuwe karibu na watoto kwa kuangalia tabia na mienendo yao kila siku”, amesisitiza Mhe. Jenista.
Aidha, Mheshimiwa Mbunge ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanaume, wanawake na watoto
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.