• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATU 45,000 wajitokeza kupima virusi vya UKIMWI ,kwa hiari

Imewekwa kuanzia tarehe: April 15th, 2020

JUMLA ya watu 45,076 wamejitokeza kupima kwa hiari virusi vya UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika kipindi cha mwaka 2019.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Evance Nachimbinya wakati anatoa taarifa ya utekelezzji wa shughuli za kudhibiti maambukizo dhidi ya virusi vya UKIMWI kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme mjini Namtumbo.

Nachimbinya amesema kati ya waliopimwa watu 587 waligundulika kuwa na maambukizi  na kwamba kiwango cha maambukizi katika Halmashauri hiyo kimepungua kutoka asilimia mbili mwaka 2018 hadi asilimia moja mwaka 2019.

Hata hivyo amesema  katika kipindi hicho wanaume ndiyo wamejitokeza kwa wingi kupima kwa hiari ambapo jumla ya wanaume 30,303 walipima kwa hiari ukilinganisha na wanawake waliokuwa 14,773.

“Wote waliobainika kuwa na maambukizi walisajiliwa katika vituo vya tiba na matunzo kwa ajili ya usimamizi wa afya zao ili kuimarisha afya zao na wapate nguvu za kuendelea kulitumikia Taifa’’,alisisitiza Nachimbinya.

Ameyataja mafanikio ambayo Halmashauri hiyo imeyapata katika kukabiliana na UKIMWI kuwa ni kutoa huduma ya tiba na matunzo kwa waishio na VVU,upimaji kufanyika katika ngazi zote za kutolea huduma za afya ili kufikia malengo ya 95 tatu kufikia mwaka 2025 na kuendelea kwa huduma ya tohara kwa wanaume.

Licha ya mafanikio hayo,amezitaja changamoto zilizojitokeza katika kipindi hicho kuwa ni kupungua kwa mchango wa wadau kutokana na kupungua kwa bajeti ya Mfadhili Mkuu  kwa serikali na changamoto ya usafiri katika vituo husika kutokana na Halmashauri kuwa na upungufu mkubwa  wa magari.

Katika kukabiliana na changamoto hizo,Mkurugenzi huyo amesema Halmashauri inashirikiana na  wadau wa shughuli za UKIMWI kama USAID BORESHA AFYA,NICE na  ZHARF katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kuhakikisha kuwa Namtumbo inakuwa salama katika maambukizi mapya ya UKIMWI.

“Wilaya ina Kamati  za kudhibiti UKIMWI katika kata 21 na vijiji 66,jumla ya kata  zinazofadhiliwa  na ZHARF zipo kumi,Halmashauri imeunda vikundi 14 vya watu waishio na virusi vya UKIMWI ambavyo vinashiriki katika uhamasishaji jamii juu ya kupima kwa hiari na utoaji  elimu namna ya kujikinga na maambukizi ‘’,alisema Nachimbinya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza mara baada ya kukagua utekelezaji wa shughuli za kudhibiti maambukizi dhidi ya virusi vya UKIMWI wilayani Namtumbo,amewapongeza wanaume kwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.

Mndeme amesema kitendo hicho kitaiwezesha serikali kufikia malengo yaliyopangwa ya kuwa na jamii salama kutokana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI  ifikapo mwaka 2030 kumaliza kabisa maambukizi.

“Hadi sasa jamii ya Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla ina uelewa wa kutosha juu ya masuala ya VVU na UKIMWI,inatambua madhara yatokanayo ya unyanyapaa na inashiriki kikamilifu katika huduma zinazotolewa za upimaji na ushauri nasaha’’,alisema Mndeme.

Hata hivyo amesisitiza kuwa mafanikio yaliyopatikana,yanaonesha kuwa jitihada zikiendelea kuchukuliwa na wadau wote wa masuala ya UKIMWI,Wilaya ya Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla,utafikia malengo ya  serikali ya kuwa na maambukizo sifuri ifikapo mwaka 2030.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Aprili 15,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.