• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATU zaidi ya 63,000 Ruvuma wanaishi na virusi vya ukimwi

Imewekwa kuanzia tarehe: December 1st, 2022

MKOA wa Ruvuma kwa mwaka 2022 unakadiriwa kuwa na zaidi ya watu 63,088  wanaoshi na Virusi vya UKIMWI.

Haya yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Ruvuma Dr.Lous Chomboko  wakati anatoa taarifa kuhusu ugonjwa wa UKIMWI kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo kimkoa yamefanyika Kata ya Luwaita wilayani Mbinga.

Dr.Chomboko amebainisha kuwa kati ya watu hao wanawake ni 37,233,wanaume ni 22,849 na Watoto ni 3,008.

“Kaulimbinu ya siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi ni Imarisha usawa,kauli hii imelenga usawa katika ngazi za familia kwa kutokuwatenga  watu wanaopata maambukizi’’,alisisitiza Dr.Chomboko.

Mganga Mkuu wa Mkoa ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa ni miongoni mwa mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI kipo juu zaidi ya kiwango cha kitaifa.

Amesema kiwango cha maambukizi ya VVU na UKIMWI mkoani Ruvuma ni  asilimia 5.6 ambapo kiwango cha kitaifa ni asilimia ni asilimia 4.7.

Hata hivyo amesema kiwango hicho cha maambukizi kimkoa kimepungua kwa asilimia 1.4 kutoka asilimia saba hadi 5.6 kwa mujibu wa  matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI na malaria kwa  mwaka 2011 hadi 2012.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya UKIMWI Duniani,Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo,amesisitiza jamii nzima kuwajali watu wenye  VVU na UKIMWI.

Amesema licha ya jitihada zote za mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI hali ya maambukizi katika Mkoa wa Ruvuma sio nzuri kwa sababu kiwango cha maambukizi kimkoa ni kikubwa zaidi ya kiwango cha maambukizi kitaifa.

“Hivyo basi inatulazimu kuendelea kujikumbusha juu ya mikakati ya mapambano dhidi ya UKIMWI ili kuendelea kupunguza maambukizi ya VVU katika Mkoa wetu’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bakari Mketo amewapongeza wadau wa afya mkoani Ruvuma kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali zinazosaidia kupunguza maambukizi mapya ya VVU ikiwemo tohara na uhamasishaji wa kupima VVU hali iliyosababisha asilimia 98.8 ya watu wanaoishi na VVU mkoani Ruvuma kujua hali zao.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Desemba Mosi,2022 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.