MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge kuongoza kutoa heshima za mwisho katika Kifo cha Mtumishi Lusian Vedastus Mwangwa.
Mgema akitoa salamu kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa watumishi katika ukumbi wa Songea Clabu amewaasa kujiandaa na kumuishi Mungu kwasababu siku za kuishi Duniani ni chache kwa kila binadamu.
“Binadamu wote ni wasafiri lakini mwisho upo japo hatujui siku na kupitia kifo cha mtumishi mwenzetu kinatukumbusha kujiweka tayari ili mwisho wa kila mmoja a uwe mwema pale umauti itakapo mfika”.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali Watu na Utawala Bakari Mketo akisoma taarifa fupi ya Marehemu huyo amesema alizaliwa Agosti 19,1969 katika Mkoa wa Mwanza na kupata Elimu ya Sekondari Azania mwaka 1987 Mkoa wa Dare es Salaamu.
Mketo amesema mwaka 1991 Juni hadi 1992 alipata mafunzo ya jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Msange iliyopo Mkoani Tabora,mwaka 1997 marehemu alimaliza Advance Diploma ya Uhasibu Chuo kikuu cha Mzumbe na mwaka 2019 alimaliza masomo ya Shahada ya Uzamili katika uendeshaji Biashara za Kimataifa kutoka Chuo cha Biashara (CBE) Dare es salaam.
Amesema Mwangwa alibahatika kufanya kazi katika ofisi mbalimbali ikiwemo kazi ya Ualimu katika shule Sekondari ya Mwandiga iliyopo Mkoani Kigoma mwaka 1992-1997 ,mwaka 1997-2006 alifanya kazi kwa ngazi ya Mhasibu msaidizi ofisi ya TRA Dare es salaam, mwaka 2006-2008 alifanya kazi Wizara ya Fedha Hazina Dare es salaam,mwaka 2008 -2009 alifanya kazi ya msajili wa vyama vya siasa Dare esa laam na mwaka 2010-2013 alifanya kazi Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi Dare es salaam.
Mketo amesema Marehemu Mwangwa alihamishiwa kikazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kupangiwa kutekeleza majukumu yake ya Uhasibu ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kuanzia Januari 29,2015 ambako amefanya kazi hadi umauti ulipo mfika.
Marehemu alifariki Dunia Machi 28,2022 kwa shinikizo la Damu (Pressure) kwa mujibu wakati akitekeleza majukumu yake katika kituo chake cha kazi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Machi 31,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.