Siku ya wafanyakazi Mkoani Ruvuma imeazimishwa katika Wilaya ya Tunduru ambapo vyama vya wafanyakazi vimepaza sauti zao kulalamikia Serikali kuhusu kikokotoo Kilichopo Kwa watumishi wa umma wakati wa kustaafu.
Akisoma Risala ya wafanyakazi Kwa Mgeni Rasmi katibu wa TUGHE Mudathiri Ismail ambaye pia ni Mratibu wa Maadhimisho hayo amesema kikokotoo hakiwahusu waajiriwa wa zamani Kwa kuwa hakikuwa katika mikataba Yao ya ajira.
Ismail katika Risala hiyo amedai wafanyakazi wanafanya tathmini ya hatima ya ajira zao wakikinyoshea kidole kikokotoo ambacho kina watesa wafanyakazi hao wanapostaafu baada ya kuitumikia serikali kwa uaminifu mkubwa .
Hata hivyo Ismail amesema kuwa mishahara ya wafanyakazi bado haikidhi mahitaji ukilinganisha na gharama halisi za maisha hivi Sasa .
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed Pamoja na mambo mengine amevishukuru vyama vya wafanyakazi Kwa kuandaa Maadhimisho hayo ya Mei Mosi na kujitokeza Kwa wingi kuhudhuria Maadhimisho hayo.
Kanali Abbas amewataka waajiri katika Mkoa wa Ruvuma kujenga mazoea ya kutoa zawadi mara kwa mara Kwa wafanyakazi ili kuongeza morali ya kufanyakazi Kwa watumishi badala ya kusubiri siku ya wafanyakazi pekee.
Mkuu wa Mkoa ameitaja migogoro ya wafanyakazi inatokana na kutozingatia misingi ya utawala Bora ,kutokuwa na ushirikishwaji, usiri usio wa lazima na uamuzi usiozingatia haki Kwa watumishi.
Hata hivyo amewapongeza wafanyakazi kupitia Risala yao kuthamini kazi kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa miradi mbalimbali Mkoani Ruvuma .
Kanali Abbas amewahakikishia wafanyakazi kuwa Changamoto zote zilizotolewa zimepokelewa na ofisi yake na Changamoto zinazoweza kutatuliwa na ofisi yake zitafanyiwa hivyo na zingine zitapelekwa katika ngazi ya kitaifa.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mwaka huu yamebeba kauli Mbiu isemayo "Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.