Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limewasimamisha kazi watumishi saba kwa tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 28. Fedha hizo zilikusanywa kupitia mashine za POS lakini hazikupelekwa benki.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Desderius Haule, alitoa maazimio ya kusimamishwa kazi kwa watumishi hao baada ya kuligeuza Baraza la Madiwani kuwa Kamati ili kuwajadili.
Pamoja na hatua hiyo, Halmashauri hiyo imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha wa serikali 2024/2025, ikikusanya zaidi ya shilingi bilioni 8.62 kutoka lengo la bilioni 8.4
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.