WAFANYAKAZI wa wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS),wameaswa kufanyakazi kwa upendo,mshikamano na kutanguliza uzalendo kwa nchi yao ili kuongeza ufanisi na huduma bora sehemu zao za kazi.
Wito huo umetolewa jana na Mhifadhi Mkuu Shamba la miti Wino mkoani Ruvuma Glory Kasmir, wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa mtumishi wa shamba hilo Theofrida Luoga iliyofanyika katika Ukumbi wa Chamali Resort unaomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania Brigedi 401 Songea.
Alisema,watumishi wakipendana na kushirikiana wanaweza kufanya mambo makubwa katika taasisi zao na kuisaidia serikali kutatua baadhi ya changamoto bila kuhitaji msaada kutoka nje na kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika kwenye idara zao.
Aidha alisema,mtumishi wa umma kufanya kazi zaidi ya miaka 50 hadi kustaafu siyo kitu kidogo na lazima kumshukuru sana Mungu kwani muda wote anakabiliwa na kukutana na changamoto nyingi ambazo wakati mwingine zinakatisha tamaa.“hadi kufikia hatua ya kustaafu katika utumishi wa umma kwa kweli lazima kushukuru Mungu,hapa katikati kuna milima na mabonde ambayo wakati mwingine yanakatisha tamaa,lakini mtumishi hautakiwi kukata tamaa bali unatakiwa kukabiliana nayo ili uendelea kutekeleza majukumu yako”alisema Kasmir.
Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti Mpepo wilayani Mbinga Misana Magayane alisema,maisha ya utumishi ndiyo marefu zaidi kuliko maisha ya nyumbani au shuleni, hivyo watumishi wanatakiwa kuishi kwa furaha na amani wakati wote.
Magayane alisema, ili mtu aishi muda mrefu katika utumishi wa umma ni muhimu kuwa amani na upendo katika utumishi wako kwa sababu hakuna binadamu aliyekamilika.
Magayane aliongeza kuwa,hata wakiletwa malaika kutoka Mbinguni bado tutawakwaza kwa kuwa malaika ni watakatifu na sisi tumelizoea kuishi na jamii ile ile inayotuzunguka kila siku ambayo ina mapungufu na madhaifu makubwa.
Kwa upande wake Theofrida Luoga, amewaomba watumishi waliobaki kukumbuka suala la kumtanguliza Mungu wakati wote katika shughuli zao,kuondoa uwoga na kutoona kufanya kazi ngumu kama sehemu ya adhabu.
Amewataka watumishi wa ngazi za chini ,kuwaheshimu viongozi wao ili kujifunza kutoka kwao namna walivyofanikiwa hadi kufika ngazi za juu za uongozi na kuacha tabia ya kushindana na kwani kufanya hivyo hakuleti mafanikio yoyote kazini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.