• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATUMISHI wa Umma Ruvuma wampongeza Rais Samia

Imewekwa kuanzia tarehe: August 29th, 2022

WATUMISHI wa kada mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazo fanya kwa kuwajali na kuridhia nyongeza ya mshahara wa kima cha chini kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma.

Walisema,kuwathamini na ongezeko la mshahara na maboresho ya maslahi mbalimbali ya watumishi yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia yanakwenda kuchochea na kuongeza morali ya uwajibikaji kwa watumishi hao.

Wametoa pongezi hizo jana mbele ya Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,walipokutana kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia kutokana na mafanikio  yake katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake.

Mdhibiti wa ubora wa shule wilaya ya Tunduru Halima Nyenje,  amempongeza  Rais Samia kwa uamuzi huo ambao utaleta ari ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma kwa kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi na wana mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa letu.

Aidha alisema, hatua ya kulipa malimbikizo,ongezeko la mishahara na maboresho yaliyofanywa na Rais Samia kwa watumishi wa umma ni ishara ya upendo wa serikali kwa watumishi wake na unapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.

Mwalimu Nyenje, amemshukuru Rais  Samia kwa  kutoa fedha nyingi kwa wilaya hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali,ikiwamo fedha zilizoletwa kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ,miradi ya maji  na sekta ya afya.

Blandina Sekela alisema kuwa,Rais Samia katika kipindi cha uongozi wake wa mwaka mmoja na miezi kadhaa ameweza kuleta nafuu na faraja kubwa kwa watumishi wa umma.Sekala ambaye ni afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya wilaya hiyo alisema,kutokana na nyongeza  hiyo ya mishahara na maboresho mengine,wananchi wategemee kupata huduma bora.

Sekela ametolea mfano,katika idara ya afya wamepata watumishi wapya 53 ambao wamepelekwa katika maeneo mbalimbali ambao wamekwenda kuongezeka kwenye baadhi ya vituo ambavyo havikuwa na watumishi wa kutosha.

Alisema,watumishi  hao watafanya kazi ya kuwahudumia wananchi kwa karibu zaidi hatua itakayowezesha sana kupunguza  vifo vya mama na mtoto kwa kuwa huduma hizo zitasogezwa karibu na wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Chiza Marando alisema,katika kipindi cha cha mwaka  2021/2022 jumla ya watumishi 139 wa kada tofauti wa Halmashauri  hiyo wamepandishwa vyeo na Serikali,kulipa kiasi cha Sh.milioni 42,468,000 kila mwezi kutokana na upandishaji wa vyeo watumishi hao.

Alieleza kuwa, katika kipindi hicho watumishi 39 wa kada tofauti wamebadilishwa vyeo ili kukidhi mahitaji ya watumishi katika idara mbalimbali na Serikali inalipa Sh.milioni 12,612,000 kila mwezi zinazotokana na kubadilishwa kada watumishi hao.

Marando alisema,watumishi  94 wa idara mbalimbali katika Halmashauri hiyo wamelipwa Sh.milioni 85,728,280 kama malimbikizo pamoja na kuajiri watumishi  123 ambao wanalipwa Sh.milioni 82,902,000 kila mwezi.

Akizungumzia kuhusu nyongeza  ya mishara iliyoanza mwezi julai mwaka huu Marando alisema,katika Halmshauri ya wilaya Tunduru mishahara imeongezeka kutoka Sh.milioni 829,973,075 hadi Sh.milioni 956,625,177.95 kwa mwezi na hivyo kufanya ongezeko la Sh. 126,652,101.95.

Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watumishi na kuwalipa maslahi yao na  jambo lililosaidia sana watumishi kufanya kazi kwa bidii ili  kutimiza azma ya Serikali ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi wa Tunduru.

Akizungumzia juu ya sensa ya watu na makazi iliyoanza leo nchini kote Marando alisema,maandalizi yamekamilika kwa asilimia 98 na hadi sasa wamepokea Sh.bilioni 1.9 kati ya bilioni 2.662,000,000 zilizopangwa kutumika kwa ajili yakufanikisha sensa ya mwaka 2022.Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro alisema, nyongeza ya asilimia 23.ya mishahara kwa watumishi wa umma,Rais Samia amezingatia kuboresha hali ya kiuchumi za watumishi wa kiwango cha chini ambao ni wengi zaidi katika kada mbalimbali  na wana viwango vidogo vya mishahara.

Alisema,Rais Samia amejipambanua  kwa kuwajali watumishi wake na kuzingatia maslahi na alianza kwa kuwaondolea kadhia ya watumishi wenye deni la mkopo wa elimu ya juu na umeleta unafuu mkubwa wa maisha kwa watumishi hao.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya,katika kipindi  cha mwaka mmoja cha uongozi wake,Rais Samia amepeleka zaidi ya Sh.bilioni 22 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii katika wilaya hiyo.

Amewataka watumishi  idara na taasisi mbalimbali za serikali kumuunga mkono Rais Samia kwa kufanya kazi kwa bidii,kumpongeza,kumshukuru na kumuombea  ili aweze kuishi maisha marefu na aendelee kutafuta fedha kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii hapa nchini.

MWISHOOOOOO.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.