DED PHILEMON MAGESA AONGOZA ZOEZI LA USAFI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA NAMTUMBO,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Philemon Magesa ameongoza zoezi la Usafi katika Kituo cha Afya cha Namtumbo kilichopo katika Kata ya Rwinga, Ikiwa ni Utekelezaji wa Maagizo ya Serikali ya Kufanya usafi wa Pamoja kati ya Wananchi na Watumishi wote katika Maeneo mbalimbali.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi wa mazingira, Magesa amewataka maafisa Afya na Mazingira kuhakikisha wanafanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya Soko na Maeneo ya Wazi ili kufanya usafi wa mazingira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.