SERIKALI Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma imesema,itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi watakaohitaji kuwekeza na kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile, baada ya kutembelea shamba la kahawa lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 3,000 linalomilikiwa na Kampuni ya Aviv Tanzania Ltd ambalo linazalisha asilimia zaidi ya tano ya kahawa inayolimwa hapa nchini.
“Kampuni ya Aviv Ltd tangu ilipoanza shughuli zake imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi,kwa mfano mwaka jana imelipa mapato ya Sh.milioni 700 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kutokana na mauzo ya kahawa,fedha hizi zimekwenda kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa Wananchi”alisema Ndile.
Alisema kuwa,hayo ni maendeleo makubwa hivyo Serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri zake itajenga na kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hao ili wasikutane na vikwazo kwa kushindwa kulipa mapato na kusababisha Halmashauri kushindwa kujiendesha.
Ndile, amesifu kahawa inayozalishwa katika shamba la Aviv Ltd lililopo kijiji cha Lipokela Halmashauri ya Wilaya Songea kuwa ni tamu ikilinganishwa na kahawa inayolimwa kwenye mikoa mingine hapa nchini kutokana na radha yake.
Alisema,Wilaya ya Songea ni kimbilio kubwa kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania wanaokwenda kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kutokana na kuwa na mazingira rafiki ikiwemo ardhi nzuri inayofaa kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara.
Kwa mujibu wa Ndile,Wilaya ya Songea ni Wilaya Mama kwa uzalishaji wa chakula katika Mkoa wa Ruvuma na ndiyo ghala kuu la Hifadhi ya Chakula Tanzania,hivyo amewaomba wawekezaji kwenda kuwekeza kwanikuna maeneo na mazingira mazuri yanayofaa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji.
Dc Ndile amemtaja mwekezaji mwingine ni kampuni ya Ndolela Farm inayofanywa shughuli zake katika Halmashauri ya Madaba ambayo imepewa hekta 500 kwa ajili ya kilimo cha zao la mahindi na ngano inayotumika kama chakula na kutengeneza bia za kampuni ya Serengeti.
“siku za nyuma kulikuwa na kasumba kwa wawekezaji kuchukua malighafi za kutengeneza bia kutoka nchini Afrika Kusini wakati hapa nchini kuna malighafi za kutosha,hali hii imewarudisha nyuma wakulima wetu na wengine kukata tamaa ya kuendelea na uzalishaji wa zao hilo”alisema.
Alisema,kampuni ya Serengeti imeingia makubaliano ya kuwapa wakulima mbegu za shahiri ambao watazalisha na kuuza kwa kampuni hiyo ambapo Halmashauri ya Madaba itapata mapato na wakulima kupata watapata fedha kutokana na kilimo cha zao hilo.
Kwa upande wake Meneja uzalishaji wa Shamba la Kahawa la Aviv Hamza Kassim alisema,wakati wa msimu wa mavuno wana ajiri watu 4,000 hadi 5,000 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Hamza alisema,uwepo wa shamba hilo unasaidia Wananchi kupata ajira za muda na ajira za kudumu na kuchangia mapato ya Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Songea,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.