• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZAZI Mbinga washauriwa kuwapeleka watoto wao shule

Imewekwa kuanzia tarehe: January 27th, 2022

WAZAZI na walezi katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wametakiwa kutumia fursa ya uwekezaji wa miundombinu katika sekta ya elimu inayofanywa na Serikali kujenga vyumba vya kisasa vya madarasa kupeleka watoto wao kupata elimu  bora.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Mbinga(Mbinga Girls)  Ifigenia Nzota,wakati wa mapokezi ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza katika shule hiyo na kuwaomba  kuhakikisha watoto wao wanafika mapema shuleni ili kuwahi muhula mpya wa masomo.
Nzota alitumia nafasi hiyo,kuwaonesha wazazi na wanafunzi  hao baadhi ya madarasa mapya yaliyojengwa na Serikali ya awamu ya sita kwa fedha za Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19.
Alisema,Shule ya Wasichana Mbinga, imejipanga kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu kwa kuhakikisha wanafunzi  wanasoma kwa vitendo ili kuwasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.

Nzota, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na  Serikali yake kwa jitihada anazofanya ikiwamo  kutafuta fedha ambazo zimetumika kujenga vyumba vipya vya madarasa na miundombinu ya elimu katika shule mbalimbali hapa nchini.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi wilayani humo, kupeleka watoto wao kusoma mapema ili waweze kunufaika na uwekezaji wa majengo mapya uliofanywa na Serikali  na walimu  waweze kutekeleza mipango yao kwa wakati na mwisho wa mwaka wapate matokeo mazuri katika masomo na mitihani yao.

Amehaidi kuwa, katika muhula wa masomo wa mwaka 2022 walimu wa shule hiyo wamejipanga kutumia fursa ya ujenzi wa madarasa mapya yaliyogharimu jumla ya Sh.milioni 41 kufundisha kwa bidii ili jitihada zilizofanywa na Serikali zilete tija sio kwa wanafunzi tu bali hata kwa Serikali ambayo imedhamiria kuinua na kuboresha elimu hapa nchini.

Mkuu huyo wa shule alisema,kiujumla hali ya kitaaluma katika shule hiyo ni nzuri  na wataendelea kufanya vizuri na kuwafanya watoto  kuwa imara na waongeze juhudi katika masomo yao kutokana na maboresho ya kitaaluma na huduma nzuri zinazotolewa.

Aidha,amewataka wanafunzi waliopangiwa kusoma katika shule hiyo, kutumia vyema fursa ya kuwepo kwa miundombinu bora ya elimu kusoma kwa bidii na kusikiliza wanachofundishwa darasani ili waweze kutumiza ndoto zao.

Amewataka  kutunza madarasa hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu, na kuepuka kufanya uharifu ambao unaweza kusababisha madarasa hayo kuchakaa mapema na kushindwa kufanikisha malengo ya Serikali yao.

Amewaomba wadau kutoka ndani na nje ya nchi, kujitokeza kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kwa kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule kama vile ujenzi wa mabweni,maabara na vifaa  ambavyo vitawezesha wanafunzi kusoma vizuri na walimu kutekeleza wajibu wao.

Baadhi ya wanafunzi walioanza kufika  kwa ajili ya kuanza safari ya masomo katika shule hiyo,wameishukuru serikali kwa kutoa fedha ambazo zimetumika kuboresha miundombinu ya elimu  na kujenga vyumba viwili vya madarasa.

Konsolatha Mkui wa kidato cha kwanza, ameishukuru Serikali kwa kujenga madarasa mazuri na kuhaidi kuwa,watatumia madarasa hayo kusoma kwa bidii na kupata matokeo mazuri katika masomo  ambayo yaitangaza shule hiyo.

Mwanafunzi mwingine Catherine Mwakalobo alisema, madarasa hayo yatapunguza tatizo kubwa la msongamano wa wanafunzi  madarasani.Hata hivyo, ameiomba Serikali  kuangalia suala la ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu ili watoto  wapate muda wa kukaa shuleni badala ya kutokea nyumbani ambako kuna changamoto nyingi.
MWISHO.



2 Attachments



 



 







Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.