Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju, amewaomba viongozi wa Serikali, Wazazi na viongozi wa dini kupitia misikiti makanisa kumlinda katika makuzi yake kuanzia tumboni hadi umri wa miaka minane.
Mpanju alikuwa anazungumza katika uzinduzi wa Progam Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) Mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Hata hivyo amesema serikali ina mpango wa kuweka mkakati wa Pamoja ili kuhakikisha wanamfikia kila mwananchi katika kupata huduma zile za msingi za afya, ulinzi, lishe na malezi chanya anayositahili kupa mtoto.
“Kama serikali tunahitaji kila mdau tuwenae na aelewe hi program ya kitaifa na aelewe nia ya serikali kwamba ni kumuokoa mtoto wa kitanzania na kutengeneza taifa bora la watu wanao wajibika na walio tayari kuifia nchi yao”, asisitiza Mpanju.
Naye, mgeni rasmi kwenye uznduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo, amewaomba wakurugenzi kupitia usimamizi wa wakuu wa Wilaya kwenda kuzindua program hiyo ngazi ya wilaya kabla ya Desemba mwaka huu.
Ameagiza Program hiyo itengewe bajeti maaalum kuanzia ngazi ya Mkoa na Halmashauri ili kufanikisha utekelezaji wake kwa urahisi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Joel Mwakapala ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwekeza mapema kwa makuzi na malezi ya mtoto ili kupunguza udumavu na utapiamlo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Odo Mwisho amesema wao kama chama wapo tayari kwenda kutoa elimu ya malezi na makuzi ya mtoto na kuwalinda dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius Mtatilo amesema malezi mabaya kwa mtoto yanasababishwa na wazazi wenyewe kwa kupitia mambo mbali mbali kwenye familia kama ugomvi ndani ya nyumba na baba kuitelekeza familia hali inayosababisha Watoto kukosa malezi bora.
Mratibu wa Programu hiyo mkoani Ruvuma ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mariam Juma amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta program hiyo nchini ambayo ina kwenda kuwasaidia watoto wote wenye umri wa miaka sifuri hadi minane hivyo kupunguza udumavu.
Imeandikwa na Farida Baruti kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Oktoba Mosi,2023
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.