Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mhifadhi Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na utalii Idara ya mambo ya Kale William Mwita ametoa rai kwa kwa watanzania kuimarisha maadili kwa vijana na kuwarithisha historia na utamaduni wa mtanzania .
Mwita Ameyasema hayo, wakati akizungumza katika kongamano la kumbukizi ya mashujaa wa vita ya majimaji lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
Mwita amesema kupitia kongamano hilo wanafikisha ujumbe waliokuwa nao babu zetu wa vita ya majimaji ambao walijitoa mhanga katika kupigania taifa hilo na kuhakikisha maadili ya Taifa yanaendelea kulindwa.
“tutatumia haya matamasha ili kuhakikisha jamii inakuwa na maadili mema na kurithisha historia kutoka kizazi kimoja kwenda kingine”, amesema Mwita.
Katika kongamano hilo Mwita amesema Mh.Rais Samia Suluhu aliwaomba machifu kuhakikisha wanatumia makongamano kama hayo kwa ajili ya kuimarisha maadili kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Kaimu Mhifadhi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Rose Kangu amesema lengo la kongamano hilo ni kuwarithisha wanafunzi mila na desturi zao ili waweze kuzishikilia.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt Julieth Kabyemerwa ameyataja maadili ya kitanzani kuwa ni nidhamu , utii, uaminifu, kutokuwa na upendeleo, kutokiuka sheria na , kuvaa mavazi yenye staa.
Kongamano la kumbukizi ya mashujaa wa vita ya majimaji hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuenzi historia na kuwarithisha vijana uzalendo uliofanywa na mashujaa hao waliopita
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.