WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ameshauri watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea kuanza kutenga maeneo yatakayosaidia wananchi kujishughulisha na utengenezaji wa Mabwawa ya ufugaji wa samaki ambayo yatachochea uchumi na kuongeza wigo wa mapato kwa Halmashauri.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea kujionea Mradi wa Shamba Darasa la Ukuzaji wa Viumbe Maji unaoendelea kujengwa na serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Kata Mpitimbi Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Waziri Mhagama ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa shamba la darasa la ukuzaji wa viumbe hai, amesema tunaweza kutumia mabwawa ya ufugaji wa samaki kama chanzo cha ajira na uchumi kwa wananchi wa Mpitimbi B.
“Mhe. Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan anamaono ya mbali sana, ametupatia mradi ambao utasaidia kuzalisha mbegu na mafunzo, tunatakiwa tuanze kujiandaa kwa kutengeneza mabwawa”.
Amefafanua mradi utakapokamilika; wananchi wawe na miundo mbinu yao ya mabwawa ya ufugaji wa samaki tayari, ili mafunzo yatakapokuwa yanafanyika wawe wanachukua vifaranga na kuweka kwenye mabwawa yao, alisema Waziri Mhagama.
Tunaweza tukatumia mikopo ya Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kuweza kutengeneza mabwawa yao ya ufugaji wa samaki, alisisitiza.
“tunapaswa tuwe na mabwawa Mengi ya samaki kushoto na kulia mwa eneo la mradi yatakayomilikiwa na vijana wakinamama na wazee ambayo samaki watafugwa kisasa na watakuwa na uzito mzuri alisema,” Waziri Mhagama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mhe. Menas Komba amesema Halmashauri inaanda andiko la kimkakati kwa ajili ya kupata fedha ya kuendeleza Lambo kubwa la maji lilopo katika kijiji cha Mpitimbi B ambalo linahitaji fedha Zaidi ya million 500.
Amefafanua kwamba ujenzi wa lambo hilo utaenda sambamba na Halmashauri kutaratibu kupitia Halmashauri ya kijiji maeneo ambayo wananchi watajenga mabwawa ya kufugia samaki, alisema
Awali katika taarifa Mhandisi Msimamizi wa Mradi, kutoka Halmashauri ya Songea Bi,Flora Tairo alisema Mradi uko katika hatua ya ukamilishwaji, kwa majengo na upandaji nyasi kwenye kingo za mabwawa. ambapo amesema mradi huo utakapokamilika utakuwa na mabwawa manne, uzio, darasa la mafunzo, stoo pamoja na maliwato.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.