Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amefungua kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali wanaohakiki kwa kina changamoto za walimu hususan upandishwaji wa vyeo.
Akifungua leo Februari 3, 2024 kikao hicho jijini Dodoma, Waziri Mchengerwa amesema katika kuhakikisha kuwa malalamiko ya Walimu yanashughulikiwa, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais UTUMISHI iliagiza Tume ya Utumishi wa Walimu kufanya uchambuzi na kubaini walimu wote wenye changamoto katika upandaji wao wa vyeo.
“Niwapongeze Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ambapo uchambuzi umefanyika na walimu zaidi ya 136,000 wamebainishwa kuwa na changamoto,
pamoja na kazi nzuri iliyofanyika, kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa malalamiko ya walimu wote yanashughulikiwa kwa ufanisi, nimeelekeza uhakiki wa kina ufanyike kwa kuhusisha taarifa za watumishi kama zilivyo kwenye Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara (HCMIS),” amesema
Ameagiza kushughulikia kikamilifu changamoto hizo ndani ya siku 14 na kufanya kazi hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuhakikisha hakuna Mwalimu anayeachwa baada ya zoezi hilo kufanyika.
Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa amewakumbusha Waajiri na Mamlaka zote zinazohudumia Walimu kusimamia vyema maslahi ya walimu ikiwa ni pamoja na kutatua kero walizo nazo.
“Naomba niweke wazi mimi sitamvumilia mtendaji yeyote ambaye hawajibiki kushughulikia kero za walimu na vilevile sitamani kusikia walimu wana malalamiko kuhusu maslahi yao ya kiutumishi,”amesema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt Charles Msonde,amesema wameamua kufanya kikao kazi cha siku 14 cha maafisa utumishi wa halmashauri ili kuhakiki taarifa za walimu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Denis Londo ,ameipongeza kazi kubwa iliyofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia ya kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.