WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawa Bora Jenista Mhagama amezindua Hotel ya Kisasa ya Canopies.
Uzinduzi huo wa Hotel umefanyika katika Kata ya Seed Ferm Manispaa ya Songea kufuatia uzinduzi wa Loyor Tour uliofanyika Agosti 15,2022 Mkoani Ruvuma .
Mhagama amempongeza mwekezaji wa Hotel hiyo Desdeliot Ruta kwa kuwekeza Mkoa wa Ruvuma na amewakaribisha wengine ambao wanaweza kuwekeza Mkoa ni hapo.
Amesema uwepo wa Hoteli kubwa utapelekea Watailii kutoka nje na ndani kutalii katika Mkoa wa Ruvuma kufuatia Mkoa wa Ruvuma na viunga vyake kuna vivutio vingi Milima ya Mtogoro,Mapango ya Chandamali pamoja na vingine vingi ambavyo vinavutia.
Akisoma taarifa ya hotel hiyo Veronica Gondwe amesema uwepo wa hotel hiyo umesabisha vijana kujipatia ajira na wamefungua fursa kwa kuuza mboga mboga Mayai,Kuku na Matunda.
Amesema Hotel hiyo ya Canopies inatarajia kufungua super Market,Minbankie na maduka ya vyakula ambavyo vitapelekea upatikanaji wa huduma kwa karibu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amesema ufunguzi wa hotel hiyo ni mwendelezo wa Loyor Tour ambao utapelekea ongezeko la Mapato katika Manispaa ya Songea
Hata hivyo amempongeza mmiliki wa hotel hiyo kwa uwekezaji na kuongeza idadi ya hotel katika Mkoa wa Ruvuma na ametoa rai kwa wawekezaji kuwa Ruvuma kuna maeneo makubwa kwaajili ya uwekezaji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 16,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.