• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI Lukuvi azindua ofisi ya ardhi Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 12th, 2020

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  amezindua ofisi ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma katika hafla ambayo imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watendaji kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma wakiwemo wakazi wa mji wa Songea,Waziri Lukuvi katika hafla hiyo pia aligawa hati miliki  kwa  baadhi ya wananchi.

Kabla ya kufunguliwa kwa ofisi hiyo wananchi wa Mkoa wa Ruvuma walikuwa wanasafiri umbali mrefu hadi mkoani Mtwara kufuatilia  kusajili Hati zao ili kupata hatimiliki.

Akitoa hotuba yake katika uzinduzi  huo Waziri Lukuvi amesema wananchi watumie ofisi hiyo na wataalamu ili kutatua changamoto za migogoro ya  ardhi iliyokuwa inajitokeza hapo mwanzo .

‘’Ofisi hii ni yenu wana Ruvuma na Wakurugenzi na mnatakiwa kuitumia ipasavyo tutaleta mitambo na kuskani majalada yenu yaliyotunzwa nyaraka mbalimbali za umilikishaji wa ardhi zote ili ziingie kwenye mfumo na ramani zote ziingie kwenye mfumo tunataka, masikini na tajiri wamilikishwe eneo na serikali ipate kodi’’,alisisitiza.

Lukuvi amesema mwananchi  wa kawaida Hati yake ikisajiliwa kwenye ofisi ya Mkoa lazima serikali impelekee  nakwamba hata wale wananchi  vijijini hati zao zimepekwe kwenye halmashauri zao.

Amemwagiza Msajili wa Hati awalasimishe maafisa ardhi ili waweze kusajili  hati hivyo kusababisha kila mwananchi kupata  hati yake kwa wakati.

‘’Nimemwagiza msajili wa hati kwamba mwananchi wa kawaida hati yake ikishatoka Mbinga na imesajiliwa ofisi za Mkoa ni marufuku kwa mwananchi huyo kufuata hati achukua katika halmashauri yake, ardhi isiwe na usumbufu tena katika kupata hati’’,alisema Lukuvi.

Lukuvi pia ametoa onyo kwa wanasheria wanaowadanganya wananchi kuwafuatilia hati zao Mtwara ili wawatapeli hela zao kwa sababu mkoa wa Ruvuma hivi sasa unatoa huduma hizo na kwamba kuanzia mwananchi anapojaza fomu  asilipe gharama yoyote.

Hata hivyo amesema katika uzinduzi huo amerudisha nyaraka zote zilizokuwepo Mtwara kabla na baada ya uhuru za mkoa wa Ruvuma za michoro na upimaji  za kumbukumbu zote na kufanya uwezeshaji mwepesi.

Waziri huyo wa Ardhi amesema kupitia ofisi ya Ardhi ya Mkoa wa Ruvuma sasa wananchi wanaweza kukopesheka na kuongeza mzunguko wa pesa katika kilimo na kukopa benki.

Imeandikwa na Anet Ndonde

Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 11,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.