Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amekabidhi vifaa tiba,jezi na vitabu vya dini katika vijiji vya Nakawale na Maniamba kata ya Kata ya Muhukuru Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Mheshimiwa Mbunge amegawa vifaa tiba katika Zahanati ya Kijiji Cha Nakawale Viti vya kutembelea wagonjwa , Mashuka, taulo za kike, Dripu Stand, vyandarua na Kitanda Cha Kujifungulia akina Mama.
Pia Mheshimiwa Jenista amewakabidhi viongozi wa dini ya kiislamu Misahafu na mikeka ya kuswalia, amegawa vifaa vya michezo (jezi na mipira) katika timu za Vijiji hivyo.
Katika Ziara hiyo Mbunge huyo ameambatana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wakuu wa Idara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.