Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Peramiho wamehimizwa Kuendelea kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuhakikisha Miradi ya maendeleo inafanikiwa na kutoa huduma sawa sawa kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama Mb) wa Peramiho wakati wa Hafla fupi ya Kukabidhi pikipiki tisa kwa Watendaji wa kata Chama Cha Mapinduzi wa kata ya Peramiho, Maposeni, Ndogosi, Kilagano, Parangu, Kizuka, Litapwasi, Muhukuru, na Mpandangindo iliyofanyika tarehe 08/07/2023 Mkoani Ruvuma.
“Vifaa hivi visaidie kukibeba chama kwanza, katika kusaidia kuongeza idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika maeneo yetu”
Ameongeza kusema Jimbo la Peramiho ni miongoni mwa Majimbo yanayofanya vizuri, katika shughuli za serikali na shughuli za chama.
Aidha Halmashauri ya Songea imepata hati safi mara mbili Mfululizo, hiyo ni ishara kwamba Uongozi wa chama na uongozi wa serikali wametambua wajibu wao, alisema Waziri Mhagama.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Songea Vijijini ametoa rai kwa Watendaji wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kuimarisha uwajibikaji na kumarisha mahusiano yao ya kiutendaji.
“Tuendelee kuwaimarisha na kuwasimamia waheshimiwa madiwani, kila mmoja kwenye eneo lake”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Mhe. Menas Komba amesema watendaji wa chama wanapaswa kuhakikisha kura za chama zinapatikana kiutendaji kwa kuhakikisha mikutano inafanyika katika ngazi ya mabalozi na ngazi ya vitongoji.
Awali Katibu Chama cha Mapinduzi Songea Vijijini Ndg, Juma Nambaila alisema moja ya eneo ambalo watalisimamia kikamilifu ni kuwapima makatibu wa kata kwa uwajibikaji wao wa shughuli za chama.
Akitoa shukrani Diwani wa kata ya Kizuka Mhe. Jackob Nditi amesema watatunza vitendea kazi na kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa chama kutekeleza maelekezo yanayotolewa na viongoz
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.