WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Mhagama amezindua mradi wa umeme Vijijini.
Uzinduzi huo umefanyika katika kijiji cha Litowa Kata ya Parangu jimboni Peramiho.
Mheshimiwa Mbunge ametoa wito kwa Wananchi kutumia vizuri mifuko ya kuwezesha upatikanaji wa mikopo ili iweze kuwasaidia kuendesha miradi mbalimbali kama kununua mashine zinazotumia umeme za kufyatulia tofali, mashine za kukamua mafuta ya alizeti au mashine za kusaga na kukoboa hivyo amewaasa kutumia umeme kufanya shughuli za maendeleo ambazo zinakuza uchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.