• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU afungua kikao kazi cha maafisa Habari Serikalini Dar es salaam

Imewekwa kuanzia tarehe: March 27th, 2023

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Maafisa Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa taarifa za jinsi serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha miaka miwili imefanya. 

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Machi 27, 2023

“Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, mnao wajibu wa kuhakikisha mnatoa taarifa za jinsi serikali ilivyotatua shida hizo za wananchi kwani kwa kutofanya hivyo wapo watu wengine wataendelea kufanya upotoshaji wakati sisi wanahabari tunajua kuwa huo ni upotoshaji.”” Alifafanua.

Alisema jukumu la kuisemea serikali ni moja ya sehemu ya mawasiliano ya nje ya serikali kwahivyo wanapaswa kuzingatia.

Alisema sambamba na hilo, aliwataka wanahabari wote wa serikali na binafsi wahakikishe wananchi wanapata elimu na  taarifa sahihi kuhusu faida na umuhimu wa miradi na mipango au shughuli zinazotelekezwa na serikali ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa sahihi kwa urahisi  zaidi na kwa wakati.

Aidha aliwataka wazingatie suala la uhuru wa kupata na kutoa habari unaoendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, Taratibu na kanuni na wadau wote kila mmoja atimize wajibu wake.

Aliwataka kuimarisha matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuongeza upatikanaji wa habari kwenye maeneo yenu.“Kila mmoja kutoka mahali alipo, tunazo taasisi za mitandao ya kijamii ambazo zinafanya kazi pamoja na serikali, endeleeni kuwashirikisha katika kutoa taarifa za kazi na shughuli za serikali.” Alisisitiza.

Pia aliwataka kushiriki kikamilifu kuitangaza vema Tanzania ndani na nje ya nchi hususan sula la amani na utulivu, fursa za biashara na uwekezaji, historia ya nchi na kuweka msisitizo katika kufuata maadili na mila za nchi na kutangaza mali kale na vivutio

Aidha aliwataka kuweka mbele uzalendo, uadilifu, uhuru na maslahi ya nchi ili kulijenga taifa na aliwakumbusha kuongeza ubunifu wa kusukuma ajenda za serikali kwa umma.

Hali kadhalika aliwataka kujiendeleza ili kuendana na asi ya mabadiliko ya kiteknlojia.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema Kikao hicho ambacho kimewaleta pamoja Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali kutoka Bara na Visiwani  ni muhimu kwa ustawi na mchango wa kada hii katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.

“Kikao hichi kitatumika pamoja na mambo mengine kutathimini mchango wetu katika kusukuma ajenda mbalimbali za serikali na namna ya kuboresha mchango huo.” Alifafanua Mhe. Nnauye.

Katika hatua nyingine TAGCO kimempa tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika kuimarisha sekta ya habari, demokrasia, uwazi, uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa nchini.

Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya TAGCO, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema,  “Sisi maafisa habari serikalini, tumemwelewa, tunamwamini na tunamuunga mkono kwa dhati, Anaishi anayoyasema na anayatenda kwa ustadi mkubwa.” Alisema Mhe. Nape

Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Mawasiliano ya Kimkakati Injini ya Maendeleo".

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.